Jinsi Rais Trump Tekelezi yataathiri wakimbizi katika Amerika?

Leo, Mahakama Kuu imesema itaruhusu Amri ya Kiutendaji ya Rais Trump kutekelezwa, kuanzia Alhamisi, Julai 29, 2017.

Amri ya Kiutendaji ilipitishwa awali na Rais Trump mwezi Januari na ilikuwa imesimamishwa kwa muda na mahakama nchini Marekani.
Mahakama Kuu ni mahakama yenye nguvu zaidi nchini Marekani. Uamuzi wao utakuwa wa mwisho ifikapo mwezi Oktoba. Uamuzi huo hautaruhusu wakimbizi kuishi nchini baada ya siku 90 zijazo na pia kuzuia watu wanaotoka nchi 6 (Iran, Libya, Somalia, Sudan, Syria na Yemen) kuingia nchini Marekani kwa siku 120 zijazo.

Uamuzi huo unaruhusu wakimbizi au watu wengine kutoka nchi 6 ambazo tayari zina uhusiano na Marekani kuendelea kuingia nchini Marekani. Kwa mfano, wakimbizi ambao wanakuja ili waishi na familia zao au watu binafsi wanaokuja kusoma katika vyuo vikuu nchini Marekani wataruhusiwa kuingia Marekani. Hatujui ni aina gani ya uhusiano ambao utatambuliwa.

Katika kipindi hicho cha siku 90, Rais Trump anasema Serikali ya Marekani itaangalia upya usalama na ulinzi uliopo katika utaratibu wa makazi nchini Marekani. Baada ya kipindi hicho, utaratibu wa makazi utaanza tena. Hata hivyo, uamuzi huu utaamuliwa na Rais Trump, serikali, na mahakama nchini Marekani.

AMRI YA RAIS TRUMP

Tangazo maalum. Kuanzia saa hii sheria ambayo ilikua imeteuliwa na mkuu wa inchi ya Marekani ( Donald Trump), iliyo kua ikihusu kuzuwiya watu au wakimbizi wanao tokea sehemu mbalimbali na kuingia katita inchi hiyo,sheria hii imebadirishwa na waamzi wakuu wa Marekani. Hii inamaanisha yakwamba kila mtu yeyote hatakama unatokea katika ichi hizi saba (Iran, Sudan, Libya, Somalia na Yemen) unaruhusiwa kuingia lakini itabidi ufuate sheria na kanuni za inchi kama ilivyo kuwa zamani. Tunawaomba watu ambao wanao tokea katika inchi hizo saba zimeandikwa juu, wasiweze kutoka inje y’Amarekani ilatu wakiwa wamepatwa nashida ambazo zinawapashwa waende kwakutatua shidahizo kwasababu Inawezekana sheria hii kubadirishwa muda wowote. Kama unandugu, jamaa au rafiki ambaye amekataliwa kuingia Marekani unaweza kupiga simu kwenye shirika hili. airport@refugeerights.org pia unaweza kupigia simu ofisi ambayo ipo karibu yako ACLU. Tunaelewa yakwamba hici nikipindi kigumu, tutaendelea na kuwajulisha jinsi mambo yanavyo endelea kubadirika. Tutajaribu kuajulisha katika lugha tofauti kwaulevu zaidi.

 

Rais Trump alitoa amri ambayo ilibadilisha sana programu ya ufanyaji upya wa makazi wa wakimbizi. Amri ya Rais ni amri itowelayo na Rais ambayo inatendeka kama sheria nchini Marekani. Kwa sababu taratibu za ufanyaji upya wa makazi ziko chini ya mamlaka ya Rais, yeye anaweza kuibadilisha programu yenyewe. Hata hivyo Amri ya Rais haiwezi kukiuka Katibu wala sheria zilizopitishwa na Bunge la Marekani.

Amri hii ya Rais ina maana gani kwa wakimbizi?

  • Amri hii inaahirisha ufanyaji makazi upya kwa muda ufuatao wa siku 120. Maana yake ni wakimbizi wowote hawatapata ruhusa kupata makazi mapya nchini Marekani kwa muda wa siku 120 zifuatazo. Huenda itasimamisha utengenezaji wa ruhusa kwa muda wa siku 120 kwa maana kutohojiwa kwa wakimbizi katika nchi za ng’ambo pamoja na upelelezi wa maisha yao ya awali pengine kutacheleweshwa.
  • Amri hiyo inaahirisha wakimbizi wote kutoka Siria kutokuja Marekani. Maana yake ni mkimbizi yeyote kutoka Siria hana ruhusa kuingia nchini Marekani hadi ambapo amri husika imebadilishwa. Hakuna muda maalum unaohusika na suala hili.

Hatujui wakimbizi wapi wataweza kuingia au lini wakimbizi wataweza kuingia Marekani ili wapate ufanyaji upya wa makazi.

Amri hii ya Rais itaniathiri mimi namna gani?

  • Ikiwa umeshakuwa mkimbizi nchini Marekani, amri hii haitakuathiria kisheria.

Hali yako ya uhalali Marekani hajabadilika. Bado unaweza kujiandikisha kupata

Kadi ya Majani baada ya muda wa mwaka mmoja wa kuwepo Marekani ukiwa mkazi.

  • Kama unamsubiri jamaa aje kukaa Marekani au kuwa pamoja nawe kwa kupitia programu ya kuungana upya kwa jamaa, labda muda umeongezeka kabla hao watakaribishwa Marekani. Ikiwa mmoja wa jamaa anatoka nchi mojawapo iliyopigwa marufuku kutoingia Marekani, ruhusa kuingia haitapatikana hadi Amri hii ya Rais imebadilika.

Endapo unahitaji msaada wa kisheria?

Kama unahitaji msaada sasa hivi kuhusu masuala ya kisheria kutokana na Amri hii ya Rais ama jamaa wakimbizi wameshapangiwa tarehe ya kuja Marekani, unaweza kuwasiliana na International Refugee Assistance Project. IRAP inaweza upatiwe na mashauri pamoja na maarifa bali haina idhini kumpatia yeyote ruhusa kuingia Marekani ambaye amepigwa marufuku na Amri ya Rais. info@refugeerights.org

Wewe unaweza kufanya nini?

Ukiwa mkimbizi, umeshatimiza shida nyingi sana. Lakini pia tunajua wewe ni mtu mwenye nguvu. Sasa hivi kuna mambo matatu unayoweza uyafanyize:

  • Kumbuka, wewe ni mtu muhimu katika maisha ya Marekani. Tunajua unachangia kwa dhati utamaduni wa nchi hii. Pia, waliowengi Wamarekani wanawakaribisha wakimbizi.
  • Kama unajisikia salaam salamini, wasimulie wengine kisa chako. Ni muhimu Wamarekani kuvifahamu wameshasikia visa vya wakimbizi wakati huu, sasa hivi.
  • Wasaidie wengine ambao hali yao ni kama yako. Wape anuani hii ya tovuti ya Refugee Center Hotline: https://therefugeecenter.org /.
  • Kama bado wewe si raia wa Marekani huku muda wako wa kukaa nchini humu unatosha, wakati ni sasa uwe raia wa Marekani. Unaweza kujiandikisha kwa Refugee Center Online free online citizenship preparation course ili kujisaidia kuwa tayari kufanya mtihani wa uraia:

classroom.therefugeecenter.org

Kama wewe ni kafara ya ubaguzi au umelengwa kwa kosa la jinai ya chuki.

Kama wewe ni kafara ya kosa la jinai, usisite kuwapigia simu polisi: 911

Kama unaamini au unamfahamu mtu aliyebaguliwa kutokana na dini au uanachama katika kundi fulani usisite kutoa ripoti: https://www.splcenter.org/reporthate

Endapo maswali mengine yangeibuka:

Ukiwa na maswali mengine, tafadhali tuma barua pepe RCO.

info@therefugeecenter.org

Nani anawapendekezea wakimbizi?

Nchini Marekani kuna kundi la nchi nzima liitwalo Refugee Council USA linalofanya kazi na Serikali kuhakikishia desturi ya heshima ya Marekani ya kuwakaribisha wakimbizi kutoka dunia nzima iendelee. Vyama vingi vinaungana na kundi hili pamoja na maofisi yote ya wakala wa ufanyaji upya wa wakimbizi. Vyama hivi vikiwa pamoja na walio wengi Wamarekani wanawaunga mkono wakimbizi.