Rais Trump alitoa amri ambayo ilibadilisha

AMRI YA RAIS TRUMP

Tangazo maalum. Kuanzia saa hii sheria ambayo ilikua imeteuliwa na mkuu wa inchi ya Marekani ( Donald Trump), iliyo kua ikihusu kuzuwiya watu au wakimbizi wanao tokea sehemu mbalimbali na kuingia katita inchi hiyo,sheria hii imebadirishwa na waamzi wakuu wa Marekani. Hii inamaanisha yakwamba kila mtu yeyote hatakama unatokea katika ichi hizi saba (Iran, Sudan, Libya, Somalia na Yemen) unaruhusiwa kuingia lakini itabidi ufuate sheria na kanuni za inchi kama ilivyo kuwa zamani. Tunawaomba watu ambao wanao tokea katika inchi hizo saba zimeandikwa juu, wasiweze kutoka inje y’Amarekani ilatu wakiwa wamepatwa nashida ambazo zinawapashwa waende kwakutatua shidahizo kwasababu  Inawezekana sheria hii kubadirishwa muda wowote. Kama unandugu, jamaa au rafiki ambaye amekataliwa kuingia Marekani unaweza kupiga simu kwenye shirika hili. airport@refugeerights.org pia unaweza kupigia simu ofisi ambayo ipo karibu yako ACLU. Tunaelewa yakwamba hici nikipindi kigumu, tutaendelea na kuwajulisha jinsi mambo yanavyo endelea kubadirika. Tutajaribu kuajulisha katika lugha tofauti kwaulevu zaidi.

 

Rais Trump alitoa amri ambayo ilibadilisha sana programu ya ufanyaji upya wa makazi wa wakimbizi.  Amri ya Rais ni amri itowelayo na Rais ambayo inatendeka kama sheria nchini Marekani.  Kwa sababu taratibu za ufanyaji upya wa makazi ziko chini ya mamlaka ya Rais, yeye anaweza kuibadilisha programu yenyewe.  Hata hivyo Amri ya Rais haiwezi kukiuka Katibu wala sheria zilizopitishwa na Bunge la Marekani.

Amri hii ya Rais ina maana gani kwa wakimbizi?

 • Amri hii inaahirisha ufanyaji makazi upya kwa muda ufuatao wa siku 120. Maana yake ni wakimbizi wowote hawatapata ruhusa kupata makazi mapya nchini Marekani kwa muda wa siku 120 zifuatazo.  Huenda itasimamisha utengenezaji wa ruhusa kwa muda wa siku 120 kwa maana kutohojiwa kwa wakimbizi katika nchi za ng’ambo pamoja na upelelezi wa maisha yao ya awali pengine kutacheleweshwa.
 • Amri hiyo inaahirisha wakimbizi wote kutoka Siria kutokuja Marekani. Maana yake ni mkimbizi yeyote kutoka Siria hana ruhusa kuingia nchini Marekani hadi ambapo amri husika imebadilishwa.  Hakuna muda maalum unaohusika na suala hili.
 • 3) Amri hii pia inapiga marufuku watu kutoka nchi fulani kutoingia Marekani kwa muda
  wa siku 90. Nchi hizi ni pamoja na Irani,  Sudani, Siria, Libya, Somalia, Yemeni. Baada ya muda wa siku 90, huenda amri hii itafutwa kwa ajili ya watu wengine. Kama wewe umetoka mojawapo ya nchi hizi afadhali kutosafiri siku hizi hata ukiwa na Kadi ya Majani. Ukiwa na jamaa au rafiki ambaye amesafiri kwenda ng’ambo akiwa na kusudi la kurudi washauri wapate mwanasheria atakayekutana nao pale kiwanja cha
  ndege wakiwasili Marekani. Tafadhali wasiliane na info@refugeerights.org.
 • Amri hii inapunguza ujumla wa wakimbizi wote watakaoweza kuja Marekani katika mwaka wa 2017, angalau idadi ya watu ingali kuwa 25,000 watakaokaribishwa.

Hatujui wakimbizi wapi wataweza kuingia au lini wakimbizi wataweza kuingia Marekani ili wapate ufanyaji upya wa makazi.

Amri hii ya Rais itaniathiri mimi namna gani?

 • Ikiwa umeshakuwa mkimbizi nchini Marekani, amri hii haitakuathiria kisheria.

Hali yako ya uhalali Marekani hajabadilika.  Bado unaweza kujiandikisha kupata

Kadi ya Majani baada ya muda wa mwaka mmoja wa kuwepo Marekani ukiwa mkazi.

 • Kama unamsubiri jamaa aje kukaa Marekani au kuwa pamoja nawe kwa kupitia programu ya kuungana upya kwa jamaa, labda muda umeongezeka kabla hao watakaribishwa Marekani. Ikiwa mmoja wa jamaa anatoka nchi mojawapo iliyopigwa marufuku kutoingia Marekani, ruhusa kuingia haitapatikana hadi Amri hii ya Rais imebadilika.

Endapo unahitaji msaada wa kisheria?

Kama unahitaji msaada sasa hivi kuhusu masuala ya kisheria kutokana na Amri hii ya Rais ama jamaa wakimbizi wameshapangiwa tarehe ya kuja Marekani, unaweza kuwasiliana na International Refugee Assistance Project.  IRAP inaweza upatiwe na mashauri pamoja na maarifa bali haina idhini kumpatia yeyote ruhusa kuingia Marekani ambaye amepigwa marufuku na Amri ya Rais.  info@refugeerights.org

Wewe unaweza kufanya nini?

Ukiwa mkimbizi, umeshatimiza shida nyingi sana.  Lakini pia tunajua wewe ni mtu mwenye nguvu.  Sasa hivi kuna mambo matatu unayoweza uyafanyize:

 • Kumbuka, wewe ni mtu muhimu katika maisha ya Marekani. Tunajua unachangia kwa dhati utamaduni wa nchi hii.  Pia, waliowengi Wamarekani wanawakaribisha wakimbizi.
 • Kama unajisikia salaam salamini, wasimulie wengine kisa chako. Ni muhimu Wamarekani kuvifahamu wameshasikia visa vya wakimbizi wakati huu, sasa hivi.
 • Wasaidie wengine ambao hali yao ni kama yako. Wape anuani hii ya tovuti ya Refugee Center Hotline:  https://therefugeecenter.org/
 • Kama bado wewe si raia wa Marekani huku muda wako wa kukaa nchini humu unatosha, wakati ni sasa uwe raia wa Marekani. Unaweza kujiandikisha kwa Refugee Center Online free online citizenship preparation course ili kujisaidia kuwa tayari kufanya mtihani wa uraia:

classroom.therefugeecenter.org

Kama wewe ni kafara ya ubaguzi au umelengwa kwa kosa la jinai ya chuki.

Kama wewe ni kafara ya kosa la jinai, usisite kuwapigia simu polisi:  911

Kama unaamini au unamfahamu mtu aliyebaguliwa kutokana na dini au uanachama katika kundi fulani usisite kutoa ripoti: https://www.splcenter.org/reporthate

Endapo maswali mengine yangeibuka:

Ukiwa na maswali mengine, tafadhali tuma barua pepe RCO.

info@therefugeecenter.org

Nani anawapendekezea wakimbizi?

Nchini Marekani kuna kundi la nchi nzima liitwalo Refugee Council USA linalofanya kazi na Serikali kuhakikishia desturi ya heshima ya Marekani ya kuwakaribisha wakimbizi kutoka dunia nzima iendelee.  Vyama vingi vinaungana na kundi hili pamoja na maofisi yote ya wakala wa ufanyaji upya wa wakimbizi.  Vyama hivi vikiwa pamoja na walio wengi Wamarekani wanawaunga mkono wakimbizi.