FAHAMU HAKI YAKO UKIWA MKIMBIZI WA MAREKANI

FAHAMU HAKI YAKO UKIWA MKIMBIZI WA MAREKANI

Taarifa zilizopo kwenye nakala hii zinakusudia kukuelimisha juu ya haki zako, haupaswi kuzihesabu kama nyaraka za kisheria zinazokutetea, lengo letu ni kutaka watu wajiandae na wala sio kuogopa, kama unaamini haki zako zimevunjwa wasiliana na mwanasheria. Ikiwa wewe au ndugu yako atahitaji msaada wowote unatakiwa au anapaswa apige simu ya dharuru kwenye namba 911.

UTANGULIZI

Tunaishi kwa wakati mgumu . Seraa hivi karibuni ndihi ya wahamiaje na wakimbizi nchini Marekani zimejenga woga miongoni mwa watu. Kama ambavyo mahakam ilivyoamua dhidi ya sera hizo kuwa kila mmoja anahaki ya kuishi ndani ya nchi hii bila kubagua wahamiaji, wakimbizi, au raia na bila kujali asili zao. Wote tunapaswa tupewe haki sawa kwa mjibu wa sheria. Makala hii imekusudia kuwaelimisha wakimbizi na wahamiaji ili kujua haki zao za msingi katika nchi hii. Makala hii haikusudii kuvijengaea woga vyombo vya dola ya Marekani, ni vizuri kufahamu kuwa  idara mbalimbali za serikali zinazosaidia watu katika matatizo mbalimbali zinapatikana nchi nzima, mfono ni idara ya polisi, wauguzi na madakitari, na idara ya zima moto. Tafadhari usisite kupiga namba ya dharura ambayo ni 911.

KILICHOBADILIKA

Tarehe 27/01/2017 Raisi wa Marekani Donald Trump alitia sahihi sera ya kuzuia wahamiaji kuingia nchini Marekani kwa mda wa miezi minne na kupunguza uandikishwaji wa wakimbizi hadi kufika idadi ya 50,000 mwaka huu. Pia alitia sahihi kwenye sera nyingine inayolenga wahamiaji waishio nchini Marekani, sera zote hizi zililenga ahadi zake alizotoa wakati wa kampeni kuwa atashughulika na uhalifu unaosababishwa na wahamiaji haramu ili hulinda usalama wa raia wa marekani.

JE, NIOGOPE?

Sera na kanuni zimeathili sana watu wengi ambao wanasubiri kuungana na familia zao wanaoishi ugaibuni. Japokuwa sera hizo haziathili moja kwa moja wakimbizi ambao tayari wanaishi nchini Marekani, ni vizuri wakimbizi na wahamiaji wote waendelee kutii sheria za nchi ya Marekani. Haupaswi kutilia mashaka uhalali wako wa kuishi ndani ya Marekani kisheria kama mkimbizi. Wakati raia wa nchi za kigeni ikiwa ni pamoja na wahamiaji halali na wakimbizi wanahesabika kuwa na haki sawa sawa na raia wa Marekani makosa madogo madogo yanayogundulika wakati wa upelelezi wa polisi kwa makundi hayo ya watu inaweza kusababishwa kupoteza uhalali wa kuishi ndani ya Marekani. Ikiwa unasubiri ndugu yako kuhamia nchini Marekani inaweza kuchukua mda kidogo pamoja na kwamba bado utatumia fursa halali ya kuwasilisha maombi ya ndugu yako katika ofisi za uhamiaji.

HAKI YAKO NYUMBANI KWAKO

Kama mawakala wa shirikisho kuja nyumbani kwangu kuzungumza na mimi

Kumekuwa na taarifa kuwa mawakala kutoka ofisi za shilikisho za upelelezi( FBI) au Idara ya usalam (DHS) kuwatemberea wakimbizi na kuzungumza nao. Ifuatavyo ndo unaweza kufanya kama kuna mtu anajaribu kuingia nyumbani kwako

·      USIFUNGUE MLANGO : Utekelezaji wa Uhamiaji au mawakala za shilikisho za upelelezi( FBI) hawawezi kuja kwako bila kibali. Kama kibali kimetolewa hangalia tarehe na saini. Kama kibali hicho kina saini ya mwanashelia na tarehe ni halali, lazima uwaache waingie ndani ila  unaweza kutumia haki yako na  kukaa kimya.

·      KAA KIMYA: kila kitu  chochote utasema kinaweza kutumika dhidi kwako mahakamani. Kwa inchi ya Marekani, una haki  ya kukaa kimya na wala kusema chochote kwa polisi. Unaweza kuwaambia kuwa unawasihi marekebisho ya 5( 5th amendment’)  na kukaa kumya.

·      ITAA MWANASHERIA :  Unaweza kupata mwanasheria kwa tovuti au unaweza kutafuta mwanasheria anaishi kwa mji wako.

·      Usi saini chochote: usi saini chochote kable ya kuongea na wakili.

·      SIMAMA KWA KUJIAMINI: Tafuta wakili mwaminifu pia shirikisha jamii ili ikutetee. Kama wewe ni kizuizini, unaweza kupata uwezo wa kupata dhamana na kutolewa, usikose matumaini.

·      Wasio raia wa Marekani, pamoja na halali wakazi , wakimbizi na asylees,kwa ujumla wote wana haki sawa na raia wa Marekani.

HAKI YAKO YA KUSAFIRI

Je naweza kusafiri nje ya Marekani nikiwa na hati ya mkimbizi( Green Card)

Kwasasa Mahakama nchini Marekani imesimamisha kwa mda sera ya kuzuia wahamiaji kutoka  kwenye nchi saba ( Iraq, Syria, Iran, Sudan, Somalia, Yemen and Libya) zinazosadikika kuwa za kiislamu, hata hivyo, wahamiaji wanashauriwa kutosafiri kuingia Marekani kwa sababu mda wowote kunaweza kutokea mabadiliko ya kisera. Kuna hatari kubwa ya kusafiri nje ya Marekani kwa ajili ya watu ambao hawana uraia wa Marekani.

·      Kama wewe ao ndugu yako yuko inje ya Marekani hakikisha unawasiliana na mwanasheria kwanza kabla ndugu yako hajaanza safari ya kurudi Marekni. Msafiri ahakikishe anahati zote za jusafiris ikiwa ni pamoja na pasipoti, Green Card au hati ya ukimbizi ya kusafiri.

·      Mkimbizi asiyekuwa na paspoti au kadi ya kijani ( Green Card) anashauriwa kutpsafiri nje ya Marekani kwa kipindi hiki kwa namna yoyote ile hata lama sio mtu wa inchi saba zilizopigwa marufuku.

·      Maaskari wa uwanja wa ndege nchini Marekani wanauwezo wa kufanya upelelezi, kuhoji kuhusu uraia wako, hati zako za kusafiria na kupekua mizigo yako

·      Ukiwa utatakiwa kuhojiwa kwenye uwanja wa ndege unayo haki ya kumtafuta mwanasheria wako wa kukuwakilisha, wanasheria wanapatikana uwanja wa ndege bila malipo kwasababu hiyo tu.

·      Kama ndugu yako au wewe mwenyewe umezuiwa au kuwekwa nchini ya uangalizi kwenye uwanja wa ndege uma haki ya kuwasiliana na:airport@refugeerights.org au wapigie  ACLU  na utoe taarifa kwa yaliyokukuta kwa kutumia hii fomu  

NI HAKI YAKO KUWA SALAMA KWA JUMIUA YAKO

Itakuwa je ikiwa mimi ni mwathirika wa unyanyasaji kwa nyumba yangu ao kwa jirani

Una haki ya kulindwa sawa sawa na raia wa Marekani kwa sababu una una hati ya ukimbizi wa Marekani. Polisi wa mji wako wapo ili kukulinda  kama mwanachama wa jumuia. Kama wewe ni mwathirika wa uhalifu unapaswa mara moja kuita polisi ( 911)

·      Kama unajisikia kama uko katika hatari, au kuna mtu anafanya vitisho dhini yako au kwa familia yako, unapaswa kuita polisi( 911) kwa haraka. Wala usikabiliane nao

·      Kama una wasiwasi kuhusu usalama wako, zungumza na mtu wa shirika ya wakimbizi au mwanasheria.

·      Kama unaamini ao kuna mtu unajua amekuwa mwathirika wa uhalifu au kubaguliwa kwa sababu ya dini yake, taifa, au kundi ya chama unapaswa kutowa ripoti hapa: https://www.splcenter.org/reporthate

Naweza kusimamia imani yangu na kuitangaza hadharani bila woga wa kukosolewa ?

Nchi Marekani una haki ya kufanya mazoezi ya dini yako. Una haki ya kuenda kuhudumu na kusikia mahubiri na mihadhara ya dini, kushiriki katika shughuli za jumuia na kuomba katika umma.

·      Kama una hofu ya ubaguzi wa dini au kulengwa kwasababu ya dini, unaweza kuwasiliana na CAIR.

KUMBUKA : sheria iko upande wako ili ikulinda

WAHAMIAJI HALALI WENYE TUHUMU ZA MAKOSA YA JINAI

·      Makosa madogo yanaweza kusababisha kufukuzwa nchini Marekani.

·      Kama wewe hujakuwa raia na umekamatwa au kuhutumiwa na uhalifu, hakikisha wakili wako anaelewa hali yako ya uhamiaji. Maombi na hatia ni kama sehemu ya kujadiliana inaweza kuhatarisha hali yako ya kisheria na inaweza kusababisha kuondolewa.

·      Kama una rekodi ya uhalifu , unapaswa kulipendekeza na kuripoti  kwa mwanasheria wako ili uelewe chaguzo yako yote.

·      Kama una uwezo wa kuweka kando uthibitisho wako, inawezekana rekodi yako ikafutwa  lakini sheria ni tofauti kwa kila mji, hivyo ni bora kushauriana na wakili wako kuhusu maswali haya.

HAKI YAKO UNAPOHOJIWA NA OFISA WA SERIKALI

Ofisa wa serikali anayo mamlaka ya kukuhoji, lakini pia unahaki ya kukataa kuhojiwa ikiwa unahisi kuwa mahojiano yatavunja haki zako za msingi, zungumza na mwanasheria wako au msimamizi wako kutoka kwenye shirika lililopewa mamlaka ya kukusaidia uwapo Marekani ili wajue namna ya kukusaidia katika mahojiano.

·      Unahaki ya kuwa na mwanasheria wa kukusaidia kwenye mahojiano

·      Unaweza kuchagua mda na mahali pa mahojiano

·      Unahaki ya kujua aina ya maswali yatakaoulizwa wakati wa mahojiano na kuwa na mtafsiri wako endapo hujui luhga ya mahojiano

·      Sio lazima ujibu maswali yote kama hujisikii kuyajibu

·      Kama unamsaidia mwanafamilia mwenzako kumleta Marekani inaweza kuchukua mda kidogo lakini bado fursa na utaratibu wa maombi ya kumleta utafutwa kama kawaida.

KUMBUKA : Hautakiwi KUTOA taarifa za uongo wakati wa mahojiano, vinginevyo itahesabika madhara kisheria

UWE MAKINI NA WAPELELEZI KUTOKA KUTOKA VYOMBO VYA SHERIA

MTEGO🙁 Entrapment )

Mtego ni hali ambayo ofisa wa serikali huweka dhini ya mtu ili kujua kama anadhamira ya uhalifu, hufanyika pale ambapo kama mtu huyo asingetegwa maana yake asingefanya kosa hilo, kwakuwa maaskari wa sirini hufuatilia kimyakimya mienendo ya waislamu na wahamiaji ndani ya nchi ya marekani ni vizuri watu wote kuishi kwa dhamira safi ili isiwepo sababu ya kuingizwa kwenye makosa ya jinai

UPELELEZI ( Surveillance)

Wewe na familia yako mnaweza kuchunguzwa na serikali, Upelelezi inaweza kufanyika kwa njia kwa njia tatu( a) Njia ya kawaida, hutokea pale ofisa wa serikali anapofuatilia taarifa za mtu kwa kutumia mtu mwingine kwenye familia.

b. Njia ya muonekano, hutumika pale ofisa wa serikali anapotumia mahojiano kwa kumhoji mmojammoja ndani ya familia ili kupata taarifa.

c. Njia ya utandawazi, hutumika kwa kutumia vifaa vya kitekinolojia kama vile simu na mitandao ya kijamii ili kupata taarifa za mawasiliano yaliyofanyika hapo nyuma. Sheria hutofuatiana kutoka State hadi State nyingine, ni vizuri kuzungumza na mwanasheria ikiwa unahisi kuwa chini ya upelelezi.

MATUMIZI  YA UTANDAWAZI

Uwe makini sana na matumizi ya utandawazi, chunga watoto wako wasiweze kufungua tovuti zinazokisiwa kuwa na utata wa kiusalama katika chi ya Marekani, sio vizuri kujadili kwenye mitandao mijadara hasi inayopelekea kuipinga serikali ya Marekani, ni vizzuri kuweka mipaka kwa watoto na vijana wako kwemye matumizi ya intanet ili waweze kufungua tovuti zenye manufaa kwao na kwa taifa. Ikiwa watoto au wazazi watakuwa wanashabikia mitazamo hasi dhidi ya serikali kuna uwezekano wa kuchunguzwa na kupelelezwa na hivyo kujikuta familia hizo zikiwa kwenye matatizo yasiyo ya lazima.

HAKI YAKO YA KUTETEA JUMUIA YAKO

Sera ya serikali imeathili sana familia za wakimbizi wengi, kama mkimbizi wewe ni mtetezi mzuri kwa wenzako, sauti yako inaweza kuwa na matunda mazuri kwasababu wewe ni mkimbizi.

Una haki ya

·      Wito na kukutana na viongozi wamechaguliwa kuongoza kwa mji wako, serikali na kwenye bunge kuendeleza uhusiano, kuwaelimisha kuhusu mchango wako katika jumuia na kuomba msaada wao kwa wakimbizi na mambo mengine yenye kulitiwa umhimu.

·      Adhitia maisha yako kama mkimbizi ili uweze kusaidia kubadilisha simulizi za wakimbizi

·      Jiunge na vikundi mbalimbali kama vile wafanyakazi makazi mapfya, viongozi wa imani, waziri, Vetarans wa kijeshi, viongozi wa wakimbizi na wanachama wa jamua kuunga mkono na kuchukua hatua kwa pamoja.

Kumbuka : Sauti yako ni mhimu sana

MAELEZO YA ZIADA & RASILIMANI

Kuna mashirika mengi ambayo anatoa habari na manufaa kuhusu haki na njisi ya kujiweka mwenyewe,kuweka  familia yako salama na jamii. Kwa bahati mbaya, pia kuna uvumi na taarifa za uongo zinazozunguka kwenye mitandao,  kama vile scams ambayo inataka kuchukua faida ya wakimbizi na wahamiaji wengine. Tafadhali hakikisha kwamba unatafuta taarifa kutoka vyanzo vya kuaminika hasa wakati unatafuta habari kwa mitandao.

Greateras1.org
The International Refugee Assistance Project
Immigrant Defense Project
Informed Immigrant
American Civil Liberties Union
Council on American-Islamic Relations
NILC
Customs & Border Protection
Refugee Resettlement Offices by State
Map of Immigration Legal Service Providers
For Schools
For Non-Profit Organizations

Thank you to Church World Service for preparing these materials to help refugees KNOW YOUR RIGHTS – REFUGEE RIGHTSYou can download this information as a PDF from Greateras1.org.

Did this page help you? Smiley face Yes Frown face No
Thank you for your feedback!